Kivumbi kinatarajiwa kutifuka mchana wa leo katika uga wa Mabaraki pale Bandari itakapokuwa mwenyeji wa AFC Leopards.
Kwenye makutano yao ya hivi majuzi walitoka sare ya 0-0.
Wakiingia kwenye mechi ya leo Bandari watakuwa na lengo la kuondoa machungu ya kichapo cha 4-0 kutoka kwa Kakamega Homeboyz.
Iwapo watashinda mechi ya leo watapunguza mwanya kati yao na viongozi wa ligi Mathare united hadi pointi tatu.
Hii ni baada ya Mathare kupewa kichapo cha 2-1 na Wanyonge Mt Kenya.
Kwenye mechi zingine hii leo. Kakamega Homeboyz wanakutana na Vihiga United, Kariobangi Sharks wanakutana na Sofapaka, Nzoia Sugar na Sony Sugar, Zoo Kericho wanakutana na KCB.
Taarifa na Dominick Mwambui.