Story by Mimuh Mohamed –
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha WIPER Balozi Chirau Ali Mwakwere ametangaza wazi azma yake ya kuwania kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022.
Katika mahojiano ya kipekee na Mwanahabari wetu Balozi Mwakwere ametoa hakikisho kwamba wakati wa utawala wake kaunti ya Kwale itaimarika zaidi kimaendeleo akipigia mfano rekodi yake nzuri ya maendeleo aliposhikilia nafasi ya ubunge wa Matuga.
Balozi Mwakwere aidha amewasihi wananchi kuchagua viongozi wenye maono ya kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa ajira badala ya kuhadaiwa na wanasiasa wanaojitafutia umaarufu kupitia kigezo cha umaskini unaowakabili.
Akigusia suala la ardhi kiongozi huyo amesema migogoro ya ardhi na tatizo la uskwota linalochangiwa na mabwenyenye kunyakua ardhi za wakaazi litatuliwa kupitia mazungumzo.