Story by: Our Correspondents
Aliyekuwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere ametangaza kujiuzulu wadhfa wake kama Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha WIPER na mwanachama wa chama hicho.
Katika mahojiano ya kipekee na Radio Kaya kwenye kipindi cha Voroni Enehu, Balozi Mwakwere amesema amechukua hatua hiyo kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi ndani ya Chama cha Wiper na itakuwa vigumu kwake kushikilia chama hicho ilhali Kirana wa Wiper Kalonzo Musyoka hakubali ushauri wa viongozi wengeni chamani.
Hata hivyo Balozi Mwakwere amekosoa mikutano ya hadhafra ya Muungano wa Azimio akisema mikutano hiyo huenda ikachangia chuki na migawanyiko ya kikabila nchini.
Wakati uo huo amesema ifikapo Februari 15 mwaka huu ataweka wazi msimamo wake wa kisiasa kwa wakenya huku akisisitiza umuhimu wa wakenya kuzingatia Katiba ya nchi na kudumisha amani.