Story by Our Correspondents–
Mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha Wiper Balozi Chirau Ali Mwakwere amepiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Zawani katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale.
Akizungumza na Wanahabari baada kutimiza jukumu lake la kikatiba la kupiga kura, Balozi Mwakwere amewasihi wakaazi wa kaunti ya Kwale kujitokeza na kushiriki zoezi hilo la upigaji kura.
Balozi Mwakwere amewasihi wakaazi wa kaunti nzima ya Kwale kuhakikisha wanapiga kura na kurudi nyumbani kusubiri matokeo ya uchaguzi ili kuzuia kushuhudiwa kwa vurugu.
Wakati uo huo amewahimiza wakenya kukumbatia swala la amani na uwiano ili kuhakikisha taifa hili linashuhudia amani.