Story by Mimuh Mohammed
Viongozi waliohudumu kama mawaziri wakati wa utawala wa Hayati Emilio Mwai Kibaki wanaendelea kutoa kauli zao kuhusu uongozi wa hayati Kibaki.
Kulingana na Balozi Chirau Ali Mwakwere, ambae alifanyakazi kama waziri wa Uchukuzi, Leba, Biashara, Mazingira na Waziri wa masuala ya kigeni chini ya utawala wa Hayati Kibaki amesema mwendazake alikuwa kiongozi aliyewapa uhuru mawaziri wake kufanya kazi pasi na muingilio wowote hali iliyofanikisha maendeleo ya taifa.
Balozi Mwakwere vile vile amesema Hayati Kibaki alikuwa kiongozi mtaratibu ,myenyekevu na alijikita zaidi katika kuwapa muongozo mawaziri wake katika kuwazesha utekelezaji wa majukumu yao.
Balozi Chirau amedokeza kwamba Hayati Kibaki wakati akiwa uongozini aliidhinisha mbinu iliyofanikisha utulivu wa kisiasa nchini.
Kwa upande wake aliyekuwa Waziri wa Kilimo wakati wa utawala wa hayati Kibaki Kipruto Arap Kirwa amesema hayati Kibaki alijitahidi kuwapa ushauri na muelekeo mawaziri wake uliowasaidia kufanikisha majukumu yao.