Story by Janet Shume-
Wahudumu wa bodaboda kutoka mjini Kwale wamefanya kikao cha pamoja na mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale Balozi Chirau Ali Mwakwere na kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta ya bodaboda katika kaunti hiyo.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Balozi Mwakwere amesema tayari ameweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha sekta ya bodaboda katika kaunti ya Kwale inaboreshwa zaidi sawa na kuinua uchumi wa kaunti hiyo.
Wakati uo huo Kiongozi huyo amedokeza kwamba iwapo wakaazi wa kaunti ya Kwale watamchagua kama gavana wa kaunti hiyo wakati wa uchaguzi mkuu basi swala la ukosefu wa ajira kwa vijana litapata suluhu la kudumu.
Kwa upande wao wahudumu wa bodaboda mjini Kwale waliohudhuria kikao hicho wameunga mkono kauli za Balozi Mwakwere huku wakilalamikia kutoangaziwa katika uongozi wa kaunti.