Waziri wa utalii nchini Najib Balala amewaonya wavamizi wa ardhi za fuo kuziregesha mara moja kabla ya kukabiliwa kisheria.
Akizungumza mjini Kilifi Balala amesema kuwa serikali haitalegeza vita dhidi ya wafisadi akisema ardhi za serikali zinapaswa kuregeshwa kwa serikali.
Naye gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amefichua kuwa eneo la Vasco Dagama Pillar hadi mto wa Sabaki litaangaziwa zaidi ikizingatiwa kwamba eneo hilo limelengwa kwa mradi wa kitalii.
Mpango huo utaendelezwa kote Pwani kulinda ardhi ya umma iliyotengewa miradi ya maendeleo.
Taarifa na Marieta Anzazi.