Story by Hussein Mdune –
Waziri wa Utalii na Wanyamapori nchini Najib Balala amesema mbuga ya wanyamapori ya Dodori katika kaunti ya Lamu itaboreshwa zaidi kwani serikali imetenga fedha zaidi za kufanikisha mpango huo.
Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Jambo-jet katika uwanja wa ndege wa Manda kaunti ya Lamu, Waziri Balala amesema hatua hiyo itaboresha sekta ya Utalii katika kaunti ya Lamu.
Waziri Balala amesema kaunti ya Lamu iko na wanyamapori wengi ambao watalii wanaweza kuzuru katika mbuga ya Dodori na kuwatazama kwani mbuga hiyo ina zaidi ya Twiga elfu nne, Nyati elfu tatu, Viboko 171,000 huku punda milia na wanyama wengine wakiwa na idadi isiyoweza kudhibitika.
Kwa upande wake Gavana wa Lamu Fahim Twaha amesema serikali ya kaunti ya Lamu imetenga shilingi milioni 45 ili kuwalipia vijana 100 watakaopewa mafunzo ya uhifadhi wa mbuga za wanyamapori katika kaunti hipo.