Waziri wa utalii nchini Najib Balala amependekeza kuhusishwa kwa ala za kitamaduni kama vile makayamba katika kutumbuiza miongoni watalii.
Balala ametaja mfumo huo kuwa bora katika kuenua sekta ya uchumi na biashara hususan kwa wapigaji wa ala hizo za miziki sawia na kufanya sherehe hizo kuwa za kienyeji.
Kwa upande wake mkurugenzi katika hoteli moja kaunti ya Mombasa Jameel Verjee akizungumza katika uzinduzi wa mtandao wa hoteli hiyo ametaja mtandao huo kurahisisha katika kuhifadhi nafasi za hoteli hiyo pindi wanapotaka.
Hata hivyo ametaja njia hiyo kuwa mwafaka katika kuenua sekta ya kibiashara hususan katika kaunti ya Mombasa.