Muigizaji Aisha Said maarufu kwa jina Maya kwenye mchezo wa kuigiza wa Maza amefichua kuwa dhulma ya kimapenzi kwa wasanii wa kike inaendelezwa humu nchini.
Aisha anayetokea kaunti ya Kwale amesema kuwa japo kwa kiasi kidogo tabia hiyo inaendelezwa na watu walio na ushawishi mkubwa katika tasnia ya uigizaji.
“Binafsi haijanitokea lakini wapo baadhi ya waigizaji wenzangu ambao hupitia changamoto hiyo,Sana sana huwa ni watu walio na ushawishi mkubwa wanafanya jambo hili ovu, ” amesema Aisha.
Aisha amewatolea mwito washikadau katika tasnia hiyo kuleta usawa kwa kuwapa wasanii nafasi sawa pasipokuwa na dhulma wala mapendeleo ya aina yoyote ile.
Taarifa na Dominick Mwambui.