Mbunge wa Jomvu kaunti ya Mombasa Badi Twalib ameitaka serikali kupitia idara husika, kuingilia kati na kukomesha unyakuzi wa ardhi katika eneo bunge hilo.
Akiongea baada ya kukutana na kamati ya ardhi katika eneo bunge lake, Badi amesema visa vya wakaazi kuhangaishwa na mabwenyenye vimezidi hali inayowafanya wakaazi kuishi kwa hofu.
Hata hivyo, Badi amewataka wakaazi kuwa makini na matapeli ili kuepuka kunyakuliwa ardhi zao, huku akiitaka kamati ya ardhi eneo hilo kuorodhesha maeneo yote yanayokumbwa na mizozo ya ardhi, ili tatizo hilo likabiliwe.
Siku ya jumamosi juma lililopita, kamishina wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki alisema kuwa wakaazi wanaojihusisha na uuzaji wa ardhi zisizokua zao watakabiliwa kisheria.
Taarifa na Hussein Mdune