Story by: Gabriel Mwaganjoni
Kutokana na lalama za ubaguzi katika utoaji wa ufadhili wa masomo katika eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa, Mbunge wa eneo hilo Badi Twalib ameliboresha zoezi hilo na kulifanya katika sehemu zilizo wazi kwa wazazi kufika na kukaguliwa stakabadhi za watoto wao.
Kulingana na Badi, ni sharti watoto wanaohitaji wanufaike na msaada huo wa kimasomo na wala sio wale walio na uwezo wa kuwalipia karo watoto wao.
Akizungumza katika eneo bunge lake la Jomvu, Badi amesema ukaguzi wa stakabadhi hizo unafanyika kwa njia ya uwazi huku akiwasihi wazazi watakaohisi kubaguliwa au kuonewa katika njia yoyote ile kuwasilisha lalama hizo kwake.
Kongozi huyo amesema ameboresha mpango huo wa ugavi wa basari ili kuwafadhili wanafunzi kutoka familia maskini kwa karo ya mwaka mzima shuleni