Picha kwa hisani –
Mbunge wa jomvu Badi Twalib ameitaka iadara ya usalama nchini kukoma kuwahamisha mara kwa mara maafisa wa polisi wanaotumwa kuhudumu katika eneo bunge hilo.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Badi amesema maafisa wanaotumwa katika eneo hilo hupewa uhamisho baada ya kuhudumu kwa kipindi kifupi,hali anayosema inatatiza juhudu za kuimarisha usalama eneo hilo.
Badi vile vile amemkosoa inspekta jenerali wa polisi nchini Hilary Mutyambai kwa madai kwamba amezembea katika kutekeleza agizo la rais Uhuru Kenyatta la kukabidhi magari kwa idara ya usalama ya eneo la jomvu.