Story by Gabriel Mwaganjoni –
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wameadhimisha swala la Eid-ul-fitr huku viongozi wa dini hiyo katika kaunti ya Mombasa wakimkosoa Kadhi mkuu nchini Sheikh Ahmed Muhdhar kutokana na tangazo lake kuhusu siku rasmi ya swala ya Eid-ul-fitr.
Viongozi hao wakiongozwa na Mweka hazina wa baraza la Maimam na Wahubiri wa humu nchini CIPK Sheikh Hassan Omar aliyewaongoza Waislamu katika kuswali swala ya Eid-ul-fitr, amesema kauli ya Kadhi mkuu inachanganya waumini wa dini ya kiislamu.
Sheikh Hassan amesema ni lazima utata huo utanzuliwe huku akimlaumu Kadhi mkuu nchini Sheikh Ahmed Muhdhar kwa kuwagawanya wafuasi wa dini ya kiislamu.
Kauli ya Skeikh Hassan imejiri baada ya siku ya Jumatano jioni Kadhi mkuu nchini kutangaza kwamba waislamu wataswali Eid siku ya Ijumaa kutokana na kutoonekana kwa mwezi.