Story by Gabriel Mwaganjoni-
Utata umezidi kugubika katika mchujo uliyokamilika wa chama cha ODM katika wadi ya Mtepeni kaunti ya Kilifi huku wafuasi wa chama hicho wakiandamana kulalamikia wizi wa kura hizo.
Wakiongozwa na Harrison Nyundo wanachama hao wa ODM wamesema mgombea wanayemuunga mkono Bazil Mwalala Mwalango alidhulumiwa na kunyimwa tiketi ya chama hicho licha ya kupata ushindi kwenye mchujo huo.
Kauli yake imeungwa mkono na Kiongozi wa kijamii eneo hilo la Mtepeni Ummi Yusuf aliyeshikilia kwamba ni lazima Bazil akabidhiwe cheti chake bila ya masharti yoyote.
Mabishano hayo yamezidi kupamba moto huku wafuasi hao wakitaka Bazil akabidhiwe cheti chake au mchujo huo uregelewe, wakiapa kujitenga na mgombea Brown Safari aliyekabidhiwa tiketi ya ODM katika kinyang’anyiro cha Wadi hiyo ya Mtepeni.