Story by Gabriel Mwaganjoni-
Kundi la Viongozi wa dini ya Kikristu linalomuunga mkono Kianara wa chama cha ODM Raila Odinga katika azma yake ya kuingia ikulu mwezi Agosti 9 limeweka wazi kwamba uwiano kati ya Odinga na Rais Uhuru Kenyatta umefanikisha mchakato wa maendeleo nchini.
Kundi hilo likiongozwa na Naibu Mwenyekiti wake Michael Kituku, limesema taifa limeshuhudia uimarishwaji wa miundo msingi na uchumi baada ya Rais Kenyatta kuungana na Raila.
Akizungumza katika Kaunti ya Mombasa, Kituku amesema sera za Raila zinaliweka taifa hili katika nafasi bora zaidi ya kukua kiuchumi.
Wakati uo huo, Kiongozi huyo wa kidini amesisitiza umuhimu wa amani katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti, 9.