Picha kwa hisani –
Story by Our Correspondents-
Baadhi ya vijana wametiwa nguvuni wakati wa zoezi la kuwasajili makurutu wa kijeshi lililoandaliwa katika eneo la Kilifi Kazkazini kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Afisa anayesimamia zoezi hilo la kuwasajili makurutu wa kijeshi Lutani Kanali Evans Oduma, vijana hao wametiwa nguvuni baada ya jaribio lao la kuwashawishi wakuu wa idara hiyo kifedha kugonga mwamba.
Akizungumza na Wanahabari, Lutani Oduma amesema tayari vijana hao wamekabidhiwa maafisa wa polisi na watafunguliwa mashtaka ya udanganyifu na kushiriki ufisadi huku akiwaonya wananchi dhidi ya kulaghaiwa na baadhi ya wakenya.
Hata hivyo, Oduma amedai kwamba zoezi hilo limefanyika vyema licha ya kushuhudiwa baadhi ya changamoto ikiwemo vijana kushindwa kustahimili mazoezi ya idara hiyo.