Picha kwa hisani –
Serikali ya kitaifa imesema kati ya wakenya milioni 37 waliosajiliwa katika mpango wa huduma namba, wakenya milioni 2.2 tayari wamepokea jumbe za kuthibitisha utayari wa kadi zao.
Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna aidha ametahadharisha kwamba wahalifu wametumia fursa ya zoezi hilo kuwatumia wakenya jumbe za utapeli akiwataka wakenya kutotuma fedha kwa matapeli hao.
Oguna aidha amesema kati ya wakenya milioni 37 waliosajiliwa,milioni 20 kati yao ni watu wazima huku milioni 17 wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 na kwamba watoto chini ya miaka 18 watapewa namba pekee bila kadi ya huduma.
Wakati uo huo Oguna ameeleza kwamba awamu ya pili ya zoezi la kusajili wakenya katika mpango wa huduma namba utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi Aprili.