DJ ameaga dunia kwa kujiua
Picha kwa hisani
Maafisa wa polisi wanachunguza kisa ambapo mcheza Santuri yaani DJ ambae ni mfanyikazi wa idhaa ya Capital Fm ameaga dunia kwa kujiua.
Ripoti zimebainisha kwamba DJ huyo Alex Nderi maarufu DJ Lithium mwenye umri wa miaka 34 alikunywa sumu usiku wa siku ya jumatano akiwa ofisini mwake.
Mwili wa mwendazake umepatikana na wafanyikazi wenzake katika ofisi za idara ya habari na Teknolojia (IT department), muda mfupi tu baada ya kunywa sumu.
Inaarifiwa kwamba marehemu Dj Lithium ameacha nyaraka yenye sababu zilizopelekea kujitoa kwake uhai, sawa na kufuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii na kuwatumia jumbe fupi watu wa karibu wa familia yake kabla ya kunywa sumu.
Maafisa wa polisi wamefika katika eneo la tukio na kuchukua sumu hio pamoja na ushahidi mwengine wakati huu ambapo uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.
Picha kwa hisani