BBI: Kenyatta na Odinga kuanza kampeni za kitaifa za kupigia debe BBI
Picha kwa hisani –
Kamati maalum ya kujadili mswada wa BBI imefichua kwamba rais Uhuru Kenyatta na mwenzake kinara wa ODM Raila odinga wataanzisha kampeni za kuipigia debe BBI kuanzia juma lijalo.
Mwenyekiti wa kamati hio ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed amesema kampeni hizo za kitaifa zitaanza tarehe moja ya mwezi ujao wa machi na ni kati ya maandalizi ya kura ya maoni itakayoandaliwa mwezi juni.
Junet amesema tayari wamebuni kamati kumi zilizopewa jukumu kuendeleza kampeni za BBI katika maeneo tofauti ya taifa,kampeni zitakazo husisha kuelimishwa kwa wananchi yaliyomo ndani ya ripoti hio.
Ameyasema haya hapo jana baada ya kufanya kikao cha faragha na viongozi wa bunge la kitaifa akiwemo kiongozi wa wengi bungeni Amos Kimunya,kiranja wa wengi Emanuel Wangwe na naibu wake Maoka Maore, pamoja na katibu wa wabunge wa jubilee mbunge wa Eldas Adan Keynan.