Adasa atanua mbawa zake.
Picha Kwa Hisani –
Msanii kutoka Mombasa Adasa anazidi kutamba na wimbo wake mpya kwa jina ‘Najidai’. Katika wimbo huo, Adasa amemshirikisha mwanamuziki maarufu na anayefanya vyema nchini na hata kimataifa Mejja pia maarufu kama Okwonko.
Wimbo huo umeonekana kupokelewa vizuri na mashabiki na kufanya vyema kwenye chati za muziki wa Pwani.
Adasa ni mwadada ambaye kazi yake kwenye tasnia ya burudani inaendelea kutambulika na wengi. Ni hivi majuzi tu, ambapo wanamuziki wengi kutoka Nairobi, Khaligraph Jones akiwa mmoja wao, walijitokeza na kummiminia sifa kem kem na kushabikia nyimbo zake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema hii leo, msanii huyo amechapisha ujumbe akiwashukuru mashabiki wake kwa kutazama wimbo huo na kuufanya kuwa nambari moja wa wiki kwenye mtandao wa Boomplay.
Kufikia sasa, wimbo huo umetazamwa na zaidi ya watu elfu 40 kwenye mtandao wa YouTube.