
Wakaazi wa tahadharishwa kutarajia mvua kubwa itakayoambatana na kimbunga-Pwani
Idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti ya Kwale imetoa tahadhari ya kushuhudiwa kwa kimbunga katika kaunti hio na kwengineko pwani kuanzia adhuhuri ya leo.
Mkurugenzi wa idara hio Dominick Mbindyo amesema kimbunga hicho kimetokona na ongezeko la joto baharini na kwa sasa kimbunga hicho kinaendelea kushuhudiwa pwani ya taifa jirani la Tanzania.
Mbindyo amesema utafiti uliofanywa na idara hio umeonyesha kwamba kimbuga hicho kitaongezeka hapo kesho na kitaandamana na mvua katika maeneo mbali mbali ya ukanda huu wa pwani.
Amesema kimbuga hicho kinatarajiwa kusababisha mawimbi makali baharini akiwataka wavuvi na wafanyibiashara katika fuo za bahari hindi kuwa makini zaidi ili kuepuka madhara ya kimbunga hicho.