Story by Hussein Mdune –
Katibu mkuu wa Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli amemkosoa Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kwa kujiunga na Naibu Rais Dkt William Ruto katika siasa zake za kuingia Ikulu.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Kilifi Atwoli amedai kwamba Mudavadi ameonyesha wazi kwamba hawezi kuwatumikia wananchi kwani ameshindwa kujitegemea kisiasa ili kupiginia nafasi ya urais.
Atwoli amemtaja Mudavadi kama ni mwanasiasa msaliti kwani ameonyesha wazi kutoshirikiana na viongozi wenza wa OKA na kujiunga na Ruto aliye Kinara wa chama cha UDA licha ya Muungano wa OKA kuwa na malengo bora kwa wakenya.
Kauli yake imejiri siku moja tu baada ya Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kuzindua rasmi safari yake ya kuwania urais katika halfa ambayo ilihudhuriwa na Naibu rais.