Story by Mwahoka Mtsumi –
Mataifa 87 yanayostawi kote ulimwenguni yatanufika na msaada wa kifedha kutoka kwa mataifa tajiri duniani kupitia mpango wa kampeni ya kusaka fedha za kuimarisha sekta ya elimu.
Akizungumza katika kikao cha pamoja kupitia njia ya mtandao ambacho kimewahusisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Westlands jijini Nairobi na wale wa Cleves Cross nchini Uingereza, Rais Uhuru Kenyatta na Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, wameahidi kwamba wanafunzi wataendelea na masomo yao kikamilifu.
Viongozi hao wawili wamesema wataekeza zaidi mikakati muafaka ya kuhakikisha sekta ya elimu inaimarishwa zaidi licha ya ulimwengu kushuhudia janga la Corona licha ya kampeni hiyo kulenga kukusanya fedha za Marekani dolla bilioni 5.
Hata hivyo mataifa yatakayonufaika na mpango huo yamehimizwa kuekeza zaidi katika sekta ya elimu huku mradi huo ukilenga kuwanufaisha zaidi ya wanafunzi bilioni moja na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne.