Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mombasa Martin Kivuva amezidi kuwakosoa viongozi wa kisiasa nchini kwa kuwagawanya Wakenya katika misingi ya kikabila.
Kivuva amesema Wanasiasa hao ndio chanzo kikuu cha chuki na mgawanyiko miongoni mwa Wakenya mashinani akiwatahadharisha Wakenya dhidi ya kuwashiriki Viongozi hao wanaipotosha jamii kwa kutumia mbinu ya ukabila.
Kulingana na Kivuva, hali hiyo imewaathiri hata watoto wadogo katika shule za msingi ambao mara nyingi hujitenga na kukumbatia marafiki wa makabila yao na kuwachukia wale wasiyokuwa wa asili yao.
Wakati uo huo, kiongozi huyo wa kidini ameitaka jamii hapa Pwani kukumbatia uiano na kujiendeleza kwa umoja na wala sio kubaguana kikabila.