Picha kwa hisani –
Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema tangu shule za humu nchini kufunguliwa mapema mwezi huu,asilimia 99 ya wanafunzi wamerejea shule kufikia sasa.
Akihutubia wanahabari akiwa eneo la Kariobangi,Magoha amesema hatua hio imetokana na ushirikiano wa wadau waliopewa jukumu la kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea shule.
Magoha amesema baadhi ya shule zimepokea asilimia 100 ya wanafunzi,akisema machifu na manaibu wao katika maeneo mbali mbali ya nchi wanaendelea kuwasaka wanafunzi ambao hawajarejea shule kufikia sasa.
Magoha amesema masomo katika shule za humu nchini yanaendelea bila changamoto zozote licha ya shule kufunguliwa wakati huu ambapo maambukizi ya corona yanaendelea kushuhudiwa nchini.