Picha kwa hisani –
Wizara ya Afya nchini imedai kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini yameongezeka hadi watu 98,334 kote nchini, hii ikiwa ni baada ya watu 63 kupata maambukizi hayo kutokana na sampuli 2,134 kufanyiwa uchunguzi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliotiwa saini na Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe, Wizara hiyo imesema kuwa watu 226 waliokuwa wakiugua virusi hivyo wamepona na kupelekea idadi hiyo kufikia watu 81,101.
Aidha Wizara hiyo imesema idadi ya watu walioaga dunia humu nchini kutokana na virusi hivyo imefikia watu 1,713 baada ya watu watatu kuthibitishwa kuaga dunia katika mda wa saa 24 zilizopita.
Wakati uo huo, Wizara ya Afya nchini imesema asilimia 93 ya watu waliothibitishwa kupata maambukizi hayo katika mda wa saa 24 zilizopita wanaugua ugongwa wa pumu.