Mshirikishi mkuu wa Ukanda wa Pwani John Elungata amesema zaidi ya asilimia 85 ya wanafunzi katika shule mbalimbali katika Ukanda wa Pwani wamerudi shuleni.
Akizungumza katika shule ya msingi ya Maji ya Chumvi kaunti ya Kwale, Elungata amesema Kaunti ya Mombasa inaongoza ikifuatiwa na ile ya Kilifi huku Kaunti za Taita taveta, Tana River na Lamu zikisajili asilimia 74.
Katika hotuba yake Elungata amesema ni sharti kila mtoto arudi shuleni wakiwemo wale waliyopachikwa mimba na waliojifungua.
Kwa upande wao Wanafunzi wa shule hiyo wamedhirisha matumaini yao ya kuendelea na masomo licha ya changamoto mbalimbali zilizochangiwa na janga la virusi vya Corona.