Asilimia 80 ya watoto wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Mombasa hawajapata matibabu maalum ili kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida.
Mwenyekiti wa Shirika linaloangazia afya ya watoto walemavu kaunti ya Mombasa Vincent Otieno amesema ni lazima watoto hao wapate huduma bora za kimatibabu kama vile kunyooshwa viungo vyao ili kuwaondolea maumivu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Haki Africa, Hussein Khalid amesema ni sharti jamii inayoishi na ulemavu katika kaunti ya Mombasa itambuliwe na kushirikishwa katika mikakati yote ya maendeleo.
Aidha amewataka wazazi walio na watoto walemavu kutafuta usaidizi ili kuhakikisha wanasajiliwa katika shule maalum za watoto walio na changamoto za kimaumbile na wapate elimu.
Taarifa Gabriel Mwaganjoni.