Story by Gabriel Mwagonjoni –
Asilimia 45 ya kesi zinazowasilishwa katika mahakama ya Mpeketoni kaunti ya Lamu zinafungamana na dhuluma za kingono na zile za kijinsia.
Hakimu mkaazi katika mahakama hiyo Eugene Pascal Nabwana amesema hali hiyo ni ya kusikitisha huku mahakama hiyo ikipokea kesi 4 au 5 kila juma zinazohusu watoto kubakwa au kulawitiwa.
Akizungumza katika eneo la Mpeketoni, Nabwana amesema cha kushangaza zaidi kuna baadhi ya wanaume wanatekeleza unyama huo kwa wanawake walio na akili taahira.
Hakimu huyo amefichua kuwa kumekuwepo na visa vya wanawake kutuhumiwa kuwalazimisha wavulana wadogo tendo la ngono akisema japo idara ya mahakama imepokea lalama hizo jamii imeogopa kuwaripoti akina mama hao.
Kwa sasa, Hakimu huyo anaendeleza vikao vya hamasa kwa jamii kuhusu dhuluma za kingono na kijinsia katika maeneo ya Mpeketoni, Witu, Chakama miongoni mwa maeneo mengine ya kaunti hiyo ya Lamu ili kuipiga vita hali hiyo.