Huku zikiwa zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya zoezi la usajili watu la Huduma namba kukamilika wakaazi kaunti ya kwale wamehimizwa kujitokeza ili wasajiliwe.
Naibu kamishna kaunti ya Kwale Dennis Baraza amesema kuwa ni asilimia 60 pekee ya wakaazi wa kaunti hiyo ambao wamesajiliwa kufikia sasa .
Amesema kuwa wakaazi wengi katika kaunti hio hawana stakabadhi zinazohitajika kusajiliwa kwenye mpango huo.
Taarifa na Rasi Mangale.