Picha Kwa Hisani –
Wizara ya Afya nchini imedokeza kuwa asilimia 25 ya watoto wa chini ya miaka mitano wana uzito duni kutokana na ukosefu wa lishe bora.
Katibu katika Wizara ya Afya nchini Dkt Rashid Aman amesema asilimia 28 ya watu wazima wa umri wa kati ya miaka 18 hadi 69 wanakabiliwana changamoto za ukosefu wa kingi mwilini kutokana kutozingatia vyakula vya lishe bora.
Akigusia takwimu za maambukizi ya virusi vya Corona, Dkt Aman amesema watu 241 wamethibitishwa kupata maambukizi hayo baada ya sampuli 4,520 kufanyiwa uchunguzi na idadi hiyo kuongezeka hadi 33,630.
Amesema kati ya watu hao 241, watu 228 ni wakenya na 47 wakiwa raia wa kigeni huku watu 152 wakiwa wanaume na 89 wakiwa wanawake na mtoton wa mwaka mmoja ni miongoni mwa walioambukizi virusi hiyo ndani ya saa 24.
Wakati uo huo amedokeza kuwa watu 66, waliokuwa wakiugua Corona wamepona na idadi hiyo kuongezeka hadi watu 19,434 huku idadi ya wale waliofariki humu nchini kutokana na virusi vya Corona ikisalia watu 567.