Picha kwa hisani –
Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amewataka Machifu wote katika eneo la Kisauni kutoa habari zinazohusu unyakuzi wa mashamba katika eneo hilo.
Kulingana na Kitiyo, Gatuzi dogo la Kisauni linashuhudia hali ya wasiwasi huku mifarakano kuhusu ardhi Ikishuhudiwa kila uchao.
Akizungumza huko Kisauni wakati wa mkutano na wadau wa usalama, Kitiyo amesema ni lazima hali hiyo idhibitiwe kabla ya kutatiza amani na utulivu katika eneo hilo.
Kitiyo amesema Gatuzi dogo la Kisauni linashuhudia utata mwingi kufuatia migogoro ya ardhi ya mara kwa mara.