Jumla ya wakaazi 1,500 katika eneo la Singila-Majengo Kaunti ya Taita taveta sasa watapata hati miliki za ardhi.
Hii ni baada ya Gavana wa Kaunti hiyo Granton Samboja kuafikiana na mmiliki wa shamba la makonge katika eneo la Mwatate kuhusu kuitenga sehemu ya ardhi yake ili kuwakimu wakaazi hao ambao wamekuwa wakiishi kama maskwota.