Mwanamume mmoja anauguza majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na wananchi waliojawa na gadhabu katika eneo la Mvumoni wadi ya Tsimba golini kaunti ya Kwale baada ya jaribio lake la kuiba vioo vya gari kutibuka.
Akithibitisha kisa hicho afisa anaesmamia kituo cha polisi cha Kwale Ludwin Sasati amesema kuwa kijana huyo ambaye hadi sasa jina lake halijatambulika amepatikana akitekeleza uovu huo akiwa na mwenzake ambaye amefanikiwa kutoroka.
Sasati aidha amesema kuwa mafisa wa polisi walipofika katika eneo la tukio kumnusuru mwanamume huyo mikononi mwa wakaazi,wamempata na vioo vinne vya magari kwenye begi lake.
Kufikia sasa visa 12 vya wizi wa vioo vya magari vimeripotiwa katika kituo cha polisi cha kwale katika muda wa majuma matatu.
Taarifa na Mariam Gao.