Picha Kwa Hisani –
Mchekeshaji kutoka Uganda Anne Kansiime ametangaza kwamba yeye na mpenzi wake Abraham Tukahiirwa ambaye ni mwanamuziki, wanatarajia mtoto wao wa kwanza.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Kansiime alipachika picha yake ambayo inaonyesha ujauzito wake akisema kwamba ametafuta njia ya kuambia mashabiki wake kuhusu habari hiyo njema kwa muda sasa.
Picha Kwa Hisani –
Pia aliahidi kuwatumbuiza mashabiki wake siku ya kesho baada ya kuwakosa kwa muda mrefu. Onyesho lake litakuwa moja kwa moja kupitia akaunti yake ya You Tube.