Picha Kwa Hisani.
Mchekeshaji na muigizaji maarufu kutoka Uganda Anne Kansiime anaomboleza kifo cha babake mzazi.
Habari za kifo chake baba yake Kansiime zilitangazwa zilitangazwa na mchekeshaji mwenzake Teacher Mpamire kupitia mitandao ya kijamii.
Kifo cha mzee huyo kinajiri miezi kadhaa baada ya kifo cha mke wake ambaye pia ni mamake Anne.
Kansiime hajapakia chochote kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha baba yake, bali mashabiki wametuma jumbe za rambirambi.