Picha Kwa Hisani.
Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka Konde Music Worldwide, Anjella amefanikiwa kupata tuzo ya kwanza kutoka kwa mtandao wa YouTube baada ya akanuti yake kufikisha wafutiliaji (subscribers) 100,000.
Angella ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Nobody’ amefikia mafanikio hayo ikiwa ni miezi mitatu tangu atangazwe rasmi kuwa chini ya lebo hiyo inayomilikiwa na Harmonize.
Baada ya kusaini mkataba aliachia wimbo wake wa kwanza uitwao ‘Kama’ aliomshirikisha Harmonize ukiwa ni wa pili kufanya pamoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Msanii huyo wa kizazi kipya, amekiri kuwa haikuwa kazi rahisi kwake kufikia mafanikio hayo pasipo upendo kutoka kwa mashabiki.
“Haikuwa kazi rahisi toka nimeianza safari yangu ya muziki rasmi nimeuona upendo wenu wa dhati mashabiki zangu ambao mmejitolea muda wenu kufuatilia kazi zangu asanteni sana upendo wenu umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu na hili limethibitika baada ya kufikisha wafatiliaji 100,000 kwenye YouTube account yangu ( silver button award ) asante sana endeleeni ku-subscribe account ya YouTube”.