Mwakilishi wa Kenya mara mbili katika mashindano ya uogeleaji ya Olympiki Jason Dunford ameingilia mziki.
Dunford aliye na umri wa miaka 32, ameingilia fani ya uimbaji wa kufoka akitambulika kwa jina “Samaki Mkuu”.
Kulingana naye alishawishiwa na msanii kutoka Mexico kwa jina Romantico kufanya mziki licha ya kusisitiza kuwa hakuwa na talanta ya mziki ndani yake.
Upokelewaji wa ngoma hiyo ijulikanayo kama “Mbaya” umekuwa mseto huku wengi wakimsuta na kumtaka kusalia katika fani ya uogeleaji. Hata hivyo wengine wamemtaka aendelee na ajiboreshe zaidi.
Swali ni kwako, Je Dunford anaweza kimziki au hana uwezo?
Tazama video hiyo hapa.
Taarifa na Dominick Mwambui.