Msanii Kaa La Moto Kiumbe amejipata kati ya mahali pagumu na jiwe baada ya kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii.
Katika picha hiyo Kaa La Moto amevalia nguo za kitamaduni huku akiwa na mzee aliye na mavazi ya kitamaduni pia.
Mzee kwenye picha hiyo anaonekana akimwaya kiasi kidogo cha pombe ya mnazi chini. Kulingana na wamijikenda hii ni ishara ya kuwakumbuka mababu zao.
Mashabiki kwenye mtandao wamenza kutupa maneno pasipokuelewa picha hiyo iliyoambatanishwa na maneno ” Komatsi Mulungu Dzulu” ilikuwa inamaana gani.
Kaa La Moto bado hajafafnua ni jambo gani lilikuwa linafanyika kwenye picha hiyo.
Taarifa na Dominick Mwambui.