Picha kwa hisani –
Aliyekuwa Waziri wa zamani humu nchini Simon Nyachae ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.
Familia ya mwendazake Nyachae, imethibitisha kifo chake na kusema kuwa marehemu alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Nyachae aliwahi hudumu katika nyadhfa mbalimbali za kiserikali nchini kama Waziri wa Kilimo, mifugo na ustawi wa uvuvi, Waziri wa Fedha na pia Waziri wa viwanda wakati wa utawala wa Hayati Daniel Arap Moi, sawia na kuhudumu kama Mbunge wa Nyaribari.
Marehemu Nyachae pia aliwahi kuhudumu katika serikali ya rais mstaafu Mwaki Kibaki, kama Waziri wa Kawi mwaka wa 2002 baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha kuwania urais kupitia chama cha Ford-Kenya ambapo baadaye alistaafu maswala ya kisiasa mwaka wa 2007.
Hata hivyo serikali imesema itawaeleza wakenya taratibu za mazishi baada ya kikao na familia ya marehemu Simoen Nyachae.