Story by Our Correspondents –
Mahakama ya kushuhulikia kesi za ufisadi nchini imemhukumu kifungo cha miaka sita gerezani aliyekuwa Waziri wa michezo nchini Hassan Wario au alipe faini ya shilingi milioni sita.
Jaji wa Mahakama hiyo Elizabeth Juma amesema ushahidi uliyowasilishwa Mahakamani umeonyesha wazi kwamba Wario alihusika katika sakata ya ufisadi ya shilingi milioni 200 za Rio Olympic mwaka wa 2016.
Katika uamuzi huo, Jaji Elizabeth ameweka wazi kwamba Wario alikosa kuzingatia usawa na uadilifu katika utendakazi wake na kuwanyanyasa baadhi ya wanariadhi walioshirika michuano ya Rio Olympic.
Naye aliyekuwa Kiongozi wa wajumbe waliotumwa kwa michuano hiyo Stephen Soy amehukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezeni au alipe faini ya shilingi milioni 103 huku wawili hao wakipewa mda wa siku 14 kukata rufaa iwapo bado hawajaridhishwa na uamuzi wa Mahakama.
Wakati wa michuano hiyo ya Rio Olympic mwaka wa 2016 iliyoandaliwa nchini Brazil, serikali ilidaiwa kutenga kima cha shilingi milioni 500 kusimamia michuano hiyo kiwango cha fedha ambacho kinadaiwa kilikuwa kingi zaidi na fedha zilizohitajika.