Story by Our Correspondents-
Rais Uhuru Kenyatta kutangaza kifo cha aliyekuwa rais wa tatu wa taifa hili Emilio Mwai Kibaki.
Kibaki amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 na ameacha watoto wanne wakiwemo Jimmy Kibaki, Judy Wanjiru, David Kagai na Tony Githinji huku akifo chake kikijiri baada ya mkewe Lucy Kibaki kufariki dunia mwaka wa 2016.
Rais Kenyatta ameagiza bendera zote nchini kupeperushwa nusu mlingoti na magari ya Naibu Rais, Jaji mkuu nchini, maspika wa mabunge yote mawili pamoja na magari ya wanadiplomasia kutowekwa bendera hadi kiongozi huyo atakapozikwa.
Hayati Kibaki aliwahi kuwa rais wa tatu wa taifa hili tangu mwaka wa 2002 hadi 2013 na aliwahi kuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa Rais wa pili wa taifa hili hayati Daniel Arap Moi tangu mwaka 1969-1982 na pia aliwahi kushikilia Wizara mbalimbali nchini ikiwemo Waziri wa fedha wakati wa utawala Mzee Jomo Kenyatta na Daniel Moi.
Kibaki alijipatia shahada ya maswala ya uchumi katika chuo cha Makarere nchini Uganda kabla ya kuelekea jijini London nchini Uingereza kwa masomo zaidi katika swala la uchumi, sayansa na siasa kabla ya kurekejea katika chuo kikuu cha Makerere kama Mhadhari mwaka wa 1956.
Kiongozi huyo atakumbukwa na wengi hasa katika swala la kuboresha uchumi wa nchi, kuimarishwa kwa demokrasia, kufanikisha mfumo wa vyama vingi na maendeleo nchini ikiwemo mpango wa ruwaza wa mwaka wa 2030, ujenzi wa barabara ya Thika highway jijini Nairobi, mpango wa mradi wa Lapset kisiwani Amu na mradi Northern Corridor sawa na ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR.
Katika swala la kisiasa, Hayati Kibaki aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha KANU mwaka wa 1963 hadi 1992, kisha akajiunga na chama cha DP mwaka wa 1992 hadi 2007 kabla ya kubuni chama cha PNU mwaka wa 2007 hadi kustaafu kwake.
Kibaki aliyezaliwa mwaka wa 1931 na aliwahi kuwa mbunge wa Othaya mwaka wa 1974 hadi 2013 kabla ya kujiondoa katika ulingo wa siasa baada ya kustaafu kama rais wa taifa hili.
Wakenya wa takaba mbalimbali wamemtaja Hayati Kibaki kama kiongozi aliyechangia mengi na atazidi kukumbwa na wengi.
Viongozi mbalimbali tajika nchini akiwemo Naibu Rais William Ruto, Kinara wa chama cha ODM Raila Odinda, Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Gavana wa Kitui Charity Ngilu, Balozi Chirau Ali Mwakwere miongoni mwa viongozi wengine ni kati ya viongozi waliotuma risala zao za rambirambi.