Taarifa na Ephie Harusi.
Kilifi, Kenya, Juni 21 – Mshukiwa wa unajisi wa mwanafunzi wa miaka 15 hatimaye amefikishwa katika Mahakama ya Kilifi baada ya kutiwa nguvuni na polisi.
Mathias Kazungu John aliyekuwa mkuu wa Itifaki katika kaunti ya Kilifi, anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mwanafunzi huyo miaka miwili iliopita na licha ya kuhitajika kuhudhuria vikao vya Mahakama jamaa huyo alikiwa akivikwepa.
Akiwa mbele ya Mahakama hiyo Hamisi Chiriba Mwachoye alikuwa mdhamani wa jamaa huyo alipofikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza, ameiomba Mahakama imuruhusu ajiondoe katika kesi hiyo kutokana na tabia ya mshukiwa huyo kukwepo vikao vya Mahakama.
Hata hivyo Hakimu Mwandamizi Justus Mulei Kituku ameagiza mshukiwa huyo kuzuiliwa Korokoroni hadi tarehe 9 mwezi Julai mwaka huu ambapo Mahakama itatoa uamuzi wake iwapo mdhamini huyo ataruhusia kujiondoa kwenye kesi hiyo.