Picha kwa hisani –
Kanisa la Kianglikana nchini Uganda limemvua cheo aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa hilo, Stanley Ntagali, na kusitisha utendaji wa majukumu ya uaskofu pamoja na kuzuiwa kuwakilisha kanisa hilo kwa madai ya uzinzi.
Askofu Ntagali alistaafu mwaka jana Machi baada ya kuhudumu kwa miaka 43 kama askofu.
Katika taarifa kwenye tovuti ya kanisa la Kianglikana mrithi wake Dkt. Stephen Samuel Kaziimba, amesema Bwana Ntagali alijihusisha na mahusiano na mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye ndoa na hilo alilifahamu.
Na kwamba alisaliti ofisi ya Askofu, kiapo alichokula wakati wa kuapishwa, na maadili mema aliyotekeleza kwa kujitolea,” Dkt. Kaziimba ameongeza.
Dkt. Kaziimba amesema kanisa la Uganda limejitolea kuwa na uwazi pamoja na kutoa wito wa maombi kwa wanandoa wote, kuomba msahama na maridhiano.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Amerika Kaskazini, Foley Beach, pia alitoa taarifa yake akionesha kusikitishwa na tukio hilo.