Picha kwa Hisani –
Aliyekua mbunge wa Garsen Danson Mungatana amekanusha madai ya kuhusika na sakata ya kupokea fedha kwa njia ya udanganyifu, akisema alikuwa katika harakati za kumuakilisha mteja wake katika shughuli za uwakili.
Mungatana anakabiliwa na madai ya kupokea fedha kutoka kwa Bi Everlyn Njoki ambaye ni Mwanakandarasi ili kumsaidia kupata zabuni katika idara ya usalama yenye thamani ya shilingi milioni 70.
Mungatana hata hivyo amesema yuko tayari kushirikiana na maafisa wa idara ya upelelezi nchini kutoa taarifa muhimu kuhusiana na sakata hiyo.