Mwanamume aliyetanda katika mitandao ya kijamii kwa kusambaza picha za wasichana wadogo akijigamba kuwanajisi hatimaye amekamatwa.
Hanga Mwazombo anayejulikana kama Bakibaki Hanga katika mtandao wa kijamii wa Facebook alionekana kusambaza picha hizo na kutusi kundi la kinamama wa Kilimani pamoja na maafisa wa polisi huku akijigamba kuwa hawezi kufanywa lolote.
Kulingana na mkurugenzi wa idara ya upelelezi kaunti ya Kilifi Said Kiprotich Muhammed, jamaa huyo mfanyikazi wa kampuni ya Wells Fargo alikamatwa hapo jana mjini Lamu anakofanyia kazi na atafikishwa katika mahakama kuu ya Malindi hivi leo ili kuwasilisha ombi la kuendelea kuzuiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Said ametoa onyo kali kwa watumizi wa mitandao ya kijamii wanaopeperusha jumbe za matusi kwamba watakabiliwa na mkono wa sheria.
Taarifa na Marieta Anzazi.