Picha kwa hisani –
Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu mawasiliano,habari na uvumbuzi imemuhoji Immaculate Kassait aliyeteuliwa kuchukua wadhfa wa kamishana wa kuhifadhi data nchini.
Akizungumza mbele ya kamati hio chini ya mwenyekiti wake mbunge wa Marakwet William Kisang ,Bi Kassait amesema kupitia uhifadhi wa taarifa muhimu za wananchi atafanikisha uimarishaji uchumi wa kidijitali.
Bi Kassait ambae awali alihudumu kama mkurugenzi wa IEBC kitengo cha kutoa mafunzo kwa wapiga kura,aliteuliwa na rais Uhuru Kenyatta juma lililopita kuchukua wadhfa huo ili kutoa nafasi kwa awamu ya pili ya mpango wa huduma namba kuanza.
Bi Kassait ambae pia alihudumu kama mkurugenzi wa usajili wa wapiga kura na msimamizi wa shughuli za uchaguzi katika tume ya IEBC kwa miaka tisa,atakua kamaishana wakwanza wa kuhifadhi data nchini iwapo kamati hio itamuidhinisha.