Picha Kwa Hisani.
Mwanamuziki nyota kutoka humu nchini, Kevin Bahati ametangaza kuachia wimbo wa kwanza kwenye albumu yake anayotarajia kuizindua siku ya Jumatatu, tarehe 14 Juni, 2021.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo alichapisha video, akieleza furaha yake wakati ambapo anatarajia kuachia mojawapo ya ngoma iliopo kwenye EP yake kwa jina ‘Love Like This’.
Bahati amejigamba kuwa hii itakuwa ni moja ya albumu bora na kubwa kuwahi kutokea hapa nchini.
“Unajua wazee wanaongea sana online wanasema ooh! nasumbua sana kwani hii ni album ya kwanza kutoka?, ni kweli hii sio ya kwanza ila hii ni album ya kwanza kubwa, Love like This”.
Aidha, mwanamuziki huyo bado hajaweka wazi ni kazi ngapi zitakamilisha albumu hiyo wala wasanii aliowashirikisha humo.