Picha Kwa Hisani
Mwanamuziki na mfanyabiashara Esther Akoth maarufu kama Akothee amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mtindo ambao umeshika kasi ulimwenguni wa wanaume kuwategemea wanawake.
Mwanamuziki huyo alionekana kutoridhia tabia ya wanaume kukubali kulipiwa ada mbali mbali na kina dada huku akionya wanawake wawe macho zaidi na swala hilo.
Aidha, aliomba msamaha kwa mashabiki wake ikiwa maneno yake yaliwakwaza na kuendelea kutilia mkazo akisema kwamba ili mwanaume achukuliwe kuwa mwanaume kamili, lazima ajukumike na wanawake ni wasaidizi tu.
Kulingana naye, hamna tatizo ikiwa mume hana kazi na mke ana kazi ila tatizo linaanza pale ambapo mwanaume anatosheka na ufukara wake na anategemea mke kwa kila jambo.
Jambo ambalo alisisitizia kina dada ni kufahamu tofauti kati ya mume na mpenzi kabla ya kuchukua maamuzi ua kumsaidia mtu kifedha.
Watu maarufu kama vile mwanamuziki Wahu Kagwi na mchekeshaji Teacher Wanjiku walijibu kwenye post hiyo ya Akothee kwa kumuunga mkono.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake wa kiume wanaonelea kwamba anapotosha kina dada wa Kenya.
Unazungumziaje kauli hii ya Akothee?